Kuhusu

Kuhusu Ibn Jariir Online Classes


Ibn Jariir Online Classes ni jukwaa la kujifunza Qur’an na masomo ya Kiislamu kwa njia ya mtandao, likilenga kuwasaidia Waislamu kujifunza dini yao kwa urahisi, ufasaha na uelewa sahihi wakiwa popote walipo.


Tunatumia teknolojia ya kisasa kufikisha elimu ya Qur’an, Tajweed, Aqeedah, Fiqh na Lugha ya Kiarabu kwa mfumo wa masomo ya moja kwa moja (live classes) pamoja na maelezo ya kina yanayomsaidia mwanafunzi kuelewa hatua kwa hatua.

Mission (Dhamira Yetu)

Kutoa elimu sahihi ya Kiislamu kwa njia ya mtandao kwa ubora wa hali ya juu, kwa kuzingatia Qur’an na Sunnah, ili kuwajenga wanafunzi wenye uelewa mzuri wa dini yao.

Vision (Maono Yetu)

Kuwa miongoni mwa majukwaa bora ya kufundisha Qur’an na elimu za Kiislamu mtandaoni katika Afrika Mashariki na duniani kwa ujumla.

Masomo Tunayotoa

Katika Ibn Jariir Online Classes tunatoa masomo yafuatayo:

• Usomaji wa Qur’an kwa Tajweed
• Hifdh (Kuhifadhi Qur’an)
• Lugha ya Kiarabu
• Aqeedah (Itikadi ya Kiislamu)
• Fiqh (Sheria za Kiislamu)
• Nahwu na Sarf
• Masomo mbalimbali ya dini ya Kiislamu

Jiunge nasi leo uanze safari ya kujifunza Qur’an na elimu ya Kiislamu kwa urahisi na mwongozo sahihi.

Bonyeza “Anza Masomo” au “Masomo” ili kuchagua kozi unayotaka.

Scroll to Top